pmbet

Rais Samia kuzindua dira ya 2050

Sisti Herman

July 8, 2025
Share :

 

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atazindua Dira ya Taifa ya 2050 Alhamisi ya Julai 17 2025, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema hayo leo Jumanne, Julai 8, 2025 katika mkutano wake na wahariri jijini Dar es Salaam.

Profesa Kitila amesema maandalizi yote ya dira hiyo yamekamilika ikiwemo kupitishwa na Baraza la Mawaziri kisha Bunge kuipokea na kuiidhinisha: "Na hii imepatiwa ulinzi tofauti na iliyopita iliishia Baraza la Mawaziri."

Amesema wananchi wa makundi mbalimbali wameshirikishwa ili kupata maoni ya Watanzania. Viongozi tofautitofauti zaidi ya 44 wamehojiwa ili kupata maoni yao.

Profesa Kitila amesema: "Dira hii 2050 ya Tanzania tuitakayo angalau itatekelezwa na marais si chini ya watatu..."

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet