Rais Ufaransa agoma Waziri Mkuu wake kujiuzulu
Sisti Herman
July 9, 2024
Share :
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amekataa ombi la Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Gabriel Attal la kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya ya chama chao bungeni.
Attal amewasilisha ombi la kujiuzulu baada ya matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge nchini humo ambapo chama chake ambacho pia ni cha Rais Macron kimeshindwa idadi ya viti vya wabunge.
Tovuti ya Sky News inaripoti kuwa Muungano wa mrengo wa kushoto wa New Popular Front (NPF) ulipata viti vingi (182), ukifuatiwa na Muungano wa Ensemble ambao Macron ni mwananchama wake ambao ulipata viti 163 na kufuatiwa na National Rally (RN) kilichopata viti 143 vya ubunge,”
“Ingawa tulikuwa na matokeo bora mara tatu kuliko ilivyotarajiwa, haimaanishi kuwa ni wengi..Kwa hivyo, kwa uaminifu kwa mila ya Republican, nitajiuzulu kesho asubuhi,” alisema waziri mkuu huyo.
Hata hivyo, Rais Macron amemtaka Attal kuendelea kubakia ofisini, ili kudhibiti hali ya amani kwa muda kutokana na viashiria vya ghasia vinavyoendelea mtaani.
Aidha Ofisi ya Rais Macron imesema Waziri Mkuu atendelea kusalia, ili kuhakikisha uthabiti wa nchi katika kipindi hichi.