Rais wa Argentina atangaza sherehe za ubingwa kimakosa
Eric Buyanza
July 20, 2026
Share :
Rais wa Argentina, Javier Milei, ameshushiwa lawama baada ya kuchapisha ujumbe kwenye mtandao wa X (zamani Twitter) uliotangaza ushindi wa timu ya taifa katika fainali ya Kombe la Dunia, huku akitangaza siku ya mapumziko kusherehekea ubingwa huo, licha ya Argentina kupoteza mchezo dhidi ya Hispania.
Ujumbe huo umezua utata mkubwa na mzaha mtandaoni, ambapo baadhi ya mashabiki wanahisi Rais alikuwa ameuandaa ujumbe huo mapema akiamini Argentina ingeshinda, kisha akasahau kuufuta baada ya timu hiyo kupoteza fainali.
Ujumbe huo ulisomeka hiviii;
"SHEREHE ZA UBINGWA WA DUNIA. Kutokana na hamasa kubwa kuhusu sherehe za mafanikio yaliyofikiwa na Timu ya Taifa ya Argentina, nawaarifu wananchi kuwa, kulingana na uamuzi wa Wachezaji na Benchi la Ufundi kuhusu siku watakayopendelea kusherehekea, siku hiyo itatangazwa kuwa mapumziko ya kitaifa."






