Rais wa Bangladesh ajiuzulu
Eric Buyanza
July 24, 2026
Share :

Rais wa Bangladesh, Mohammed Shahabuddin, amejiuzulu wadhifa wake wakati hali ya kisiasa nchini humo ikiendelea kuwa tete.
Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu Sheikh Hasina kutangaza kuwa ana mpango wa kurejea Bangladesh, licha ya kukabiliwa na kesi zinazoweza kumpelekea adhabu ya kifo kufuatia ukandamizaji wa maandamano yaliyoongozwa na wanafunzi mwaka 2024, yaliyosababisha kuanguka kwa serikali yake.
Kwa mujibu wa taarifa, Shahabuddin alikuwa akikabiliwa na shinikizo la kujiuzulu kutoka kwa viongozi wa chama tawala cha upinzani, huku barua yake ya kujiuzulu ikieleza kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na matatizo ya afya.
Barua hiyo tayari imewasilishwa kwa Spika wa Bunge, Hafiz Uddin Ahmad, kwa hatua zaidi.
Source:BBC





