pmbet

Rais wa Burundi asema mashoga 'wanapaswa kupigwa mawe'

Eric Buyanza

December 30, 2023
Share :

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amesema wapenzi wa jinsi moja nchini Burundi "wanapaswa kupigwa mawe" na kwamba hiyo haitakuwa uhalifu.
 

Rais alisema hayo katika mkutano na waandishi wa habari jana (Ijumaa).
 

Akijibu swali la mwandishi wa habari, alisema nchi zenye nguvu duniani "zinapaswa kubaki" na misaada yao kwa Burundi ikiwa misaada hiyo inaambatana na masharti ya kutoa haki kwa wapenzi wa jinsi moja.
 

Alitumia maandiko ya biblia kusema kwamba Mungu anachukia mapenzi ya jinsia moja na kusema kwamba suala hilo halina mjadala nchini Burundi.
 

"Kwangu mimi, nadhani ikiwa tutapata watu hawa nchini Burundi wanapaswa kupelekwa kwenye viwanja vya michezo na kupigwa mawe, na kufanya hivyo haitakuwa kosa," rais alisema.
 

Bw Ndayishimiye alisema uhusiano wa jinsia moja ni kama "kuchagua kati ya Shetani na Mungu".
 

"Ikiwa unataka kumchagua Shetani sasa nenda ukaishi katika nchi hizo, na nadhani wale wanaojitahidi kwenda huko wanataka kuiga tabia hizo, wanapaswa kubaki huko na kamwe wasituletee," rais aliongeza.
 

Mapenzi ya jinsi moja ni kinyume cha sheria nchini Burundi na adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka miwili jela.
 

Mwezi Agosti mwaka huu, watu saba walihukumiwa vifungo vya kati ya mwaka mmoja na miwili baada ya mahakama katika mji mkuu wa kisiasa Gitega kuwapata na hatia ya kushisriki mapenzi ya aina hiyo, walikanusha mashtaka.

 

Source: BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet