pmbet

Rais wa FIFA akoshwa na uwezo wa wachezaji kutupia magoli.

Joyce Shedrack

June 26, 2026
Share :

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Gian Infantino amesifu mtindo wa soka la kushambulia pamoja na ubora wa wachezaji katika kutumia nafasi na kufunga mabao, akisema kuwa hayo ndiyo yamechangia kufikiwa kwa rekodi kubwa ya mabao katika Kombe la Dunia 2026.

FIFA bất ngờ muốn đổi luật giữa World Cup, Chủ tịch Infantino lên tiếng về  tranh cãi

Hadi kufikia mwisho wa michezo ya hatua ya makundi iliyochezwa tarehe 25 Juni 2026, jumla ya mabao 175 yalikuwa tayari yamefungwa, yakivunja rekodi ya mabao 172 yaliyofungwa katika mashindano yote ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

 

Katika ujumbe wake, Rais huyo aliwapongeza pia wachezaji wote waliofanikiwa kufunga mabao katika mashindano hayo, akisisitiza mchango wao mkubwa katika kuongeza burudani na ushindani wa michuano hiyo.

 

“Hongereni kwa wafungaji wote, na ninatarajia kuona mabao mengi zaidi kadri tunavyoelekea kwenye fainali itakayochezwa Jumapili, tarehe 19 Julai, mjini New York New Jersey,” alisema Rais wa Fifa

 

Kauli hiyo imekuja wakati mashindano yakiendelea kuvutia dunia kwa ushindani mkali na idadi kubwa ya mabao, huku mashabiki wakitarajia mechi za hatua za mwisho kuendelea kutoa burudani ya hali ya juu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet