Rais wa FIFA ampongeza Rais wa TFF kwa kuchaguliwa tena.
Joyce Shedrack
August 19, 2025
Share :
Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gianni Infantino ametuma salama za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa kuchaguliwa tena kuongoza nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka minne.
Kupitia taarifa iliyotolewa leo na TFF imesema Rais Infantino amempongeza pia Makamu wa Rais, pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa katika uchaguzi huo.
Aidha,Amemshukuru Rais Karia kwa juhudi, kazi na mchango wake muhimu katika maendeleo ya mpira wa miguu pamoja na kusimamia thamani yake na kumtakia heri na mafanikio.