Rais wa Iran afariki kwenye ajali ya Helikopta
Eric Buyanza
May 20, 2024
Share :
Rais wa Iran Ebrahim Raisi, Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo na wengine wamepatikana wakiwa wamekufa katika ajali ya helikopta, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya serikali.
Vyombo vya habari vya serikali vimeripoti kuwa watu wote tisa waliokuwa kwenye helikopta hiyo wamefariki wakati Helikopta hiyo ilipoanguka katika jimbo la kaskazini-magharibi mwa Azerbaijan la Iran.
Raisi na Waziri wa Mambo ya Nje Amir Abdollahian walikuwa wakisafiri kurudi kutoka kwenye mkutano na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev.
Helikopta hiyo ilitoweka kwenye rada Jumapili mchana.
Televisheni ya taifa ya Iran imeripoti kuwa "hakuna dalili ya mtu aliye hai" katika eneo la ajali ya helikopta iliyombeba Rais Ebrahim Raisi na wengine.
"Baada ya kupata helikopta hiyo, hapakuwa na dalili zozote za abiria wa helikopta kuwa hai hadi sasa," imeongeza ripoti hiyo.
Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti kwamba waliokua safarini na rais katika helikopta hiyo ni waziri wa mambo ya nje wa Iran Hussein Amirabdollahian, Gavana wa jimbo la Azerbaijan Mashariki Malek Rahmati na abiria wengine kadhaa.
DW