Rais wa Kenya aomba radhi kwa Taifa la Tanzania.
Joyce Shedrack
May 28, 2025
Share :
Rais wa Kenya William Ruto ameliomba radhi Taifa la Tanzania kama kuna makosa yoyote ambayo wameyafanya kwa Tanzania kwa njia yoyote ile.
Rais Ruto amezungumza hayo akitoa hotuba katika maombi ya kuliombea Taifa la Kenya siku ya leo yaliyofanyika katika katika Hotel ya Safari Park Jijini Nairobi.
āMajirani zetu Tanzania kama tumewakosea kwa njia yoyote tafadhali mtusameheāAmesema Rais Ruto huku akiomba radhi pia kwa Taifa la Uganda akisema āKwa marafiki zetu Uganda kama kuna chochote kibaya ambacho Wakenya wamefanya,Mtusameheā.