Rais wa Marekani Joe Biden akutwa na virusi vya Covid
Eric Buyanza
July 18, 2024
Share :
Rais Joe Biden wa Marekani amekutwa na virusi vya Covid-19, lakini Ikulu ya Marekani imeripoti kuwa dalili alizonazo sio kali sana na alipatiwa dozi yake ya kwanza ya dawa ya kupambana na virusi hivyo iitwayo Paxlovid,
Daktari wake, Kevin O'Connor, alisema Rais Biden alianza kuonyesha dalili za matatizo ya kupumua, ikiwa ni pamoja na mafua na kikohozi.
Bwana Biden baadaye alitumia mtandao wa X, kumshukuru kila aliyemtakia afya njema na akasema atahakikisha kazi ya wamarekani inafanyika wakati akiendelea kupona.