pmbet

Rais wa Nigeria atajwa na FBI tuhuma za dawa za Kulevya

Sisti Herman

September 6, 2026
Share :

 

Shirika la Ujasusi la Marekani, FBI imethibitisha kuwa Rais Bola Tinubu alikuwa akichunguzwa kwa tuhuma za uhalifu wa biashara ya dawa za kulevya mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Hii ni kwa mujibu wa tamko lililowasilishwa mahakamani chini ya kiapo katika mahakama ya shirikisho ya Marekani.

Tamko hilo liliwasilishwa tarehe 28 Agosti 2026, katika Mahakama ya Columbia, likiwa sehemu ya kesi inayoendelea chini ya Sheria ya Uhuru wa Kupata Taarifa (FOIA) inayolenga kupata rekodi za FBI zinazomhusu Tinubu.

Katika nyaraka hizo, FBI ilieleza kuwa "rekodi husika zilikusanywa wakati wa uchunguzi uliofanywa na FBI dhidi ya watu kadhaa kwa tuhuma za uhalifu wa biashara ya dawa za kulevya."

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet