Rais wa PSG atamani mbape aendelee kubaki
Eric Buyanza
January 10, 2024
Share :
Rais wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi, anasema ana hamu kubwa ya kuendelea kumuona mshambuliaji Kylian Mbappe akiendelea kusalia kwenye kikosi cha mabingwa hao wa Ufaransa.
Al-Khelaifi anaamini Paris St-Germain bado ndio klabu bora kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye kandarasi yake kwenye klabu hiyo inamalizika msimu wa majira ya joto.