Rais wa Ufaransa, Emir wa Qatar wamuita Mbappe Ikulu
Sisti Herman
February 28, 2024
Share :
Mshambualiaji wa PSG anayemaliza mkataba wake Kylian Mbappé jana usiku amekutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani kwenye ikulu ya Ufaransa “Elysée Palace”.
Licha mjadala wao kutokuwa wazi lakini Rais wa Ufaransa alisikika akimwambia Mbappe "Utatuletea matatizo zaidi", Macron alimwambia Mbappé huku akitabasamu.
Mbappé na mkataba wake sio mada ya mkutano huu, kwani Kylian tayari ameamua kuondoka PSG na inatajwa kuwa ana asilimia kubwa ya kujiunga na klabu ya Real Madrid.