pmbet

Rais Zelensky aapa kulipiza yaliyofanywa na Urusi

Eric Buyanza

January 9, 2024
Share :

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema mashambulizi ya Urusi hayapaswi kufumbiwa macho bila kujibiwa.
 

Katika hotuba yake aliyoitowa kwa njia ya video jana jioni, kiongozi huyo wa Ukraine amesema magaidi wanapaswa kulipia gharama ya uharibifu uliosababishwa na kitendo cha ugaidi na Urusi itawajibika.
 

Watu wanne waliuwawa na wengine 45 walijeruhiwa katika miji ya Kharkiv, Zaporizhzhya na Khmelnytskyi jana Jumatatu.
 

Zelensky pia amebaini kwamba majadiliano na washirika wa kimataifa wa Ukraine yatakayofanyika wiki kadhaa zijazo yatajikita katika kuimarisha ulinzi wa anga wa nchi hiyo.
 

Jana Urusi ilivurumisha msururu wa makombora pamoja na mashambulizi ya kutumia droni kuelekea Ukraine.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet