Ram Chauhan: Mwanaume mwenye sharubu ndefu zaidi duniani
Eric Buyanza
May 18, 2024
Share :
Ram Singh Chauhan, anayetokea Rajasthan nchini India ndiye mwanaume anayeshikilia rekodi ya dunia ya Guiness ya kuwa masharubu marefu zaidi duniani, yenye urefu wa futi 14.
Chauhan, anasema sharubu zake ndicho kitu cha thamani zaidi kwake na ametumia miaka 32 kuitunza mpaka kufikia hapo.
“Kukuza masharubu ni kama kumtunza mtoto, unahitaji kuyalea kweli kweli…imenichukua muda mrefu sana kuifikisha hadi futi 14. Haikuwa kazi rahisi” anasema Bwana Ram.