pmbet

Ramadhan Brothers wapata mapokezi ya kipekee

Eric Buyanza

March 9, 2024
Share :

Wasanii wa sarakasi kutoka Tanzania, Ibrahim na Fadhili Ramadhan wanaounda kundi la The Ramadhan Brothers wamereja Tanzania jana Machi 08,2024 wakitokea Marekani ambako hivi karibuni walishinda katika mashindano ya kusaka vipaji ya ‘America’s Got Talent Fantasy League’ na kujinyakulia Dola 250,000 (Sh milioni 637.5) pamoja na tuzo.

Wasanii hao ambao walipokelewa na Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na BASATA, wametua Uwanja wa Ndege wa Mwl. JK Nyerere Dar es Salaam ambapo ndege waliyosafiri nao imemwagiwa maji (water salute) ikiwa ni ishara ya heshima kwa Wasanii hao kwa kuiheshimisha na kuitangaza Tanzania.

Ramadhani Brothers ambao walishiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza mwaka 2023 kwenye msimu wa 18 wa America’s Got Talent na kushika nafasi ya 5, wamewahi pia kushiriki mashindano mengine ya kimataifa katika Nchi za Ujerumani, Slovakia, Ufaransa , Australia pamoja na Marekani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet