pmbet

Ramaphosa kuiaga Bafana Bafana Mei 27 kuelekea kombe la dunia

Eric Buyanza

May 25, 2026
Share :

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa,Mei 27, 2026, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa chakula cha ya jioni cha Timu ya Taifa ya nchi hiyo, kwa ajili ya Maandalizi ya Kombe la Dunia, katika Ukumbi wa Wageni wa Rais, Sefako M. Makgatho mjini Pretoria.

 

Dhifa hiyo ya chakula cha jioni ina kaulimbiu ya United by Hope, Driven by Pride" itatumika kukiaga kikosi cha timu ya taifa Bafana Bafana, kabla ya kuelekea kwenye michuano ya Kombe la Dunia la FIFA huko Mexico, Marekani na Kanada.

 

Hafla hiyo pia itajumuisha kutangazwa kwa kikosi cha mwisho cha wachezaji 26 na Kocha Mkuu wa Bafana Bafana, Bw Hugo Broos.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet