pmbet

Ramovic athibitisha Ikangalombo hayupo fiti kuivaa Kengold.

Joyce Shedrack

February 4, 2025
Share :

Kocha wa Mkuu wa klabu ya Yanga Sead Ramovic akizungumza kuelekea mchezo wao wa Februari 05 dhidi ya Ken Gold amethibitisha kuwa nyota wao mpya Jonathan Ikangalombo Kapela hatakuwa sehemu ya kikosi chao kwenye mchezo huo kutokana na kukosa utimamu mzuri wa mwili.

 

Ramovic ameonekana kuridhishwa na kiwango cha mchezaji huyo huku akiweka wazi kuwa hawawezi  kumchezesha kwa sasa wakihofia majeraha kwa mchezaji.

"Jonathan ni mchezaji mzuri sana, jambo la kwanza tunalopaswa kufanya, bila shaka, ni kumfikisha kwenye kiwango cha utimamu wa mwili tunachotaka. Kwa sababu si tu kuhusu utimamu wa mwili, bali pia kuhakikisha kwamba hapati majeraha”

“Ikiwa hana utimamu wa kutosha na anahitaji kukimbia kwa kasi kwenye mechi, kuna uwezekano mkubwa wa kuumia, na hilo ndilo tunalotaka kuepuka. Lakini bila shaka yeye ni mchezaji mzuri na katika siku zijazo atatusaidia sana"-Sead Ramovic Kocha wa Yanga

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet