pmbet

Rap haitakuwa na amani, daima kutakuwa na ushindani - Drake

Eric Buyanza

April 9, 2024
Share :

Mkali wa muziki wa hip-hop duniani Drake ambaye kwasasa yuko kwenye ziara, amesema tasnia ya muziki wa rap haitakuwa na amani hata siku moja.

Drake anasema siku zote kwenye muziki huo kutakuwa na ushindani, na kama ushindani utaendelea kuwepo basi hakutakuwa na amani kamwe.

Rapa huyo raia Canada mwenye makazi yake nchini Marekani alionyesha taarifa hiyo kwenye ubao wake wa ujumbe wakati wa ziara yake.

Taarifa hiyo ilisomeka, “Mchezo wa Rap hautakuwa na amani kamwe. Siku zote kutakuwa na ushindani. Na kama kutakuwa ushindani basi hakutakuwa na amani kamwe. Kwasababu kila mmoja atataka aonekane yeye yuko juu kuliko wenzake.” ilisomeka taarifa hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet