Rapa 2 Chainz apata ajali ya gari
Eric Buyanza
December 10, 2023
Share :
Rapa kutoka nchini Marekani, 2 Chainz alikimbizwa hospitali huko Miami usiku wa jana baada ya kuhusika kwenye ajali ya gari iliyohusisha magari matatu likiwemo na lake.
Rapa huyo wa miaka 46 ambaye jina halisi ni Tauheed Epps alishare picha instagram story akiwa anapakizwa ndani ya gari la wagonjwa (Ambulance)
Taarifa zinasema Rapa huyo alipata ajali hiyo akiwa anatoka kwenye club ya usiku, na amepata majeraha kwenye shingo lakini anaendelea vizuri.