Rapa achora tattoo ya mpenzi wake aliye jela
Sisti Herman
January 28, 2024
Share :
Rapa Chrisean Rock ameonyesha kumkumbuka mzazi mwenzake Rapa Blueface ambaye yupo jela kwa sasa. Chrisean amechapisha video Ikimuomesha akiwa na tattoo ya Blueface usoni na kuandika ujumbe akitaka Blueface aachiwe huru
Blueface anatumikia kifungo cha zaidi ya miezi 6 jela ya Los Angeles kwa kosa la kukiuka masharti ya dhamana katika mashtaka yake ya kuhusika kwenye tukio la upigaji wa risasi huko Las Vegas 2022 lakini pia kumshambulia baunsa katika Club ya Los Angeles 2021
Hivyo ameripotiwa kuwa atakaa jela hadi msimu wa majira ya joto (Julai 2, 2024).