Rapa Julio Foolio auawa kwa risasi nje ya hoteli
Eric Buyanza
June 24, 2024
Share :
Rapa wa Florida nchini Marekani, Julio Foolio ameuawa na watu wasiojulikana kwa kupigwa risasi usiku wa Jumapii nje ya hoteli huko Tampa.
Polisi wanasema waliitwa eneo la tukio baada ya raia kusikia milio ya risasi saa 10 na dk 40 ya alfajiri siku ya Jumapili.
Baada ya kuwasili, askari walikuta magari mawili kwenye maegesho yakiwa yamepigwa risasi yakiwa na watu wanne waliojeruhiwa, akiwemo mmoja aliyetambulika kwa jina la Charles Jones (Julio Foolio), ambaye alifikwa na umauti muda mchache baadae kabla hajaondolewa eneo la tukio.