Rapa maarufu wa Iran ahukumiwa kifo kwa kuunga mkono maandamano
Eric Buyanza
April 25, 2024
Share :
Mahakama ya mapinduzi ya Iran imemhukumu kifo mwanamuziki (Rapa) maarufu nchini humo, Toomaj Salehi kwa mashtaka yanayohusiana na maandamano ya mwaka 2022-2023, wakili wake ameliambia gazeti la Sharq.
Salehi katika nyimbo zake aliunga mkono maandamano ya miezi kadhaa nchini Iran mwaka 2022 yaliyosababishwa na kifo cha mwanadada Mahsa Amini akiwa mikononi mwa polisi. Mahsa Amini aliyekuwa na umri wa miaka 22 alikamatwa kwa madai ya kuvaa Hijab "isivyostahili".