Rapa Marekani atumbuiza ngoma ya Rayvanny.
Joyce Shedrack
July 10, 2024
Share :
Msanii kutoka nchini Marekani aliyejipatia umaarufu kupitia mtandao wa Instagram Dream Doll ametumbuiza wimbo wa msanii wa Bongo Fleva Rayvanny uitwao ‘Shake shake’ nchini Uingereza alipokuwa kwenye show yake.
Mwanamuziki huyo ambaye alishawahi kutamba na ngoma kama Watchu like, Who you loving, Different, Ice cream dream, Everthings Nice, You know my Body na nyingine nyingi amechapisha video kupitia Insta story yake akiwa anatumbuiza wimbo huo Jijini London.
Ikumbukwe mwezi mei mwaka jana wimbo wa ‘shake shake’ ulitoka rasmi ambapo Dream Doll alishirikishwa na Chui baadhi ya mistari na mpaka sasa unawatazamaji Milioni 1.