Rapa Tekashi akutwa na madawa ya kulevya na bastola nyumbani kwake.
Joyce Shedrack
April 22, 2025
Share :
Kulingana na ripoti Rapa Tekashi 6ix9ine anaweza kukabiliwa na majanga makubwa baada ya maajenti wa upelelezi kuripoti kupata madawa ya kulevya na bastola wakati walipokuwa kwenye uvamizi wa Machi nyumbani kwake Florida.
Mahakamani rapa huyo aliomba msamaha lakini akasisitiza kwamba alikuwa na rafiki yake wa zamani ndiye aliyepanda vitu hivyo na si vya kwake .
Wakili wake anasema wana imani kwamba kesi hiyo itatatuliwa kwa niaba ya 6ix9ine.
Mara ya mwisho rapa huyo alitoka jela kwa kupunguziwa kifungo kwa ahadi ya kutaja magenge ya uhalifu yaliyobakia ,ikiwa ni kesi iliyompeleka gerezani novemba mwaka jana.