pmbet

Rapa wa Iran aachiwa huru baada ya hukumu ya kifo kubatilishwa

Eric Buyanza

December 2, 2024
Share :

Mwanamuziki wa muziki wa Rap kutoka nchini Iran anayefahamika kwa jina la Toomaj Salehi ambaye alihukumiwa kifo kwa kuunga mkono maandamano dhidi ya serikali ameachiliwa huru baada ya kukaa gerezani kwa miaka miwili.

Rapa huyo alikamatwa Oktoba mwaka 2022 baada ya kuunga mkono maandamano yaliyozuka kote nchini Iran kufuatia kifo cha mwanadada Mahsa Amini akiwa mikononi mwa polisi.

Hukumu ya Toomaj ilibatilishwa mwezi Juni na akaachiliwa kutoka gerezani siku ya Jumapili "baada ya kutumikia kifungo cha mwaka mmoja kwa propaganda dhidi ya serikali.

Salehi, 34, aliwakosoa viongozi wa Iran katika muziki wake na alikuwa tayari amepigwa marufuku kutumbuiza kwenye tamasha kabla ya kukamatwa kwake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet