Raphinha aondoka Brazil arejea Barcelona kisa tatizo la misuli.
Joyce Shedrack
September 30, 2026
Share :
Raphinha ameondolewa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Brazil na kurejea Barcelona baada ya vipimo kubaini kuwa ana uvimbe mdogo wa misuli nyuma ya paja la kulia.

Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) limeeleza kuwa uamuzi huo umechukuliwa kama tahadhari ili kumpa Nahodha wao nafasi ya kupona vizuri.
Nyota huyo wa FC Barcelona alitolewa nje kipindi cha pili katika ushindi wa Brazil 4-2 dhidi ya Australia, baada ya kuhisi maumivu katika paja la kulia muda mchache baada ya kufunga bao la Brazil kwa mkwaju wa penalti.
Kwa sasa, taarifa rasmi hazijaonyesha kuwa ni jeraha kubwa au la muda mrefu Brazil imeamua kutomjumuisha kwenye mchezo ujao dhidi ya India huku pia ikithibitisha kwamba haitamuita mchezaji mwingine kuchukua nafasi yake.
Uamuzi huu unafanyika pia kutokana na historia ya Raphinha ya matatizo ya misuli hivyo Brazil na Barcelona wameamua kutokuweka hatari yoyote isiyo ya lazima.





