pmbet

Raphinha apata maumivu ya misuli baada ya kutupia Brazil.

Joyce Shedrack

September 29, 2026
Share :

Nyota wa Barcelona na Brazil Raphael Belolli maarufu Raphinha ametolewa kipindi cha pili katika mchezo wa kirafiki kati ya Brazil na Australia, baada ya kupata tatizo la misuli. 

Barcelona captain Raphinha suffers thigh discomfort during Australia  friendly - Yahoo Sports

 

Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) limethibitisha kuwa mchezaji huyo alihisi tatizo, hivyo benchi la ufundi likachukua uamuzi wa kutomuweka kwenye hatari zaidi.

 

Kabla ya kuondolewa, Raphinha alikuwa na mchango muhimu katika mchezo huo akifunga bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penalti kabla ya mapumziko, na kusaidia Brazil kuibuka na ushinda wa mabao 4-2 katika mchezo huo.

 

Raphinha ametoka kwenye kipindi kizuri akiwa na Barcelona, ambapo amefunga hat-trick mbili mfululizo na kufikisha mabao 14 katika mechi nane za mwanzo za msimu.

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet