Raphinha ashinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu Hispania.
Joyce Shedrack
June 6, 2025
Share :
Mchezaji wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Brazil Raphael Belloli maarufu Raphinha ametangazwa rasmi kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Hispania laliga msimu wa 2024/25.

Nyota huyo ambaye alionesha kiwango bora msimu uliopita na kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa Nchi hiyo amemaliza msimu akiwa amefunga jumla ya magoli 18 na kutoa pasi 9 za magoli katika michezo 36 aliyocheza.
Raphinha anaungana na Lamine Yamal kutoka safu ya ushambuliaji ya Hans Flick ambao wamefanikiwa kutwaa tuzo za ligi kuu nchini humo mpaka sasa.