Raphinha kureje uwanjani dhidi ya Osasuna.
Joyce Shedrack
May 2, 2026
Share :
Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na Nahodha wa timu hiyo Raphael Belloli maarufu Raphinha anatarajia kurejea kwenye kikosi katika mchezo wa ligi dhidi ya Ossasuna baada ya kukosa mwezi mzima wa Aprili kutokana na majeraha.

Zikiwa zimesalia mechi tano kabla ya msimu kumalizika, mshambuliaji huyo mwenye uzoefu anaweza kuwa na mchango mkubwa wakati timu yake ikijaribu kudumisha uongozi wao wa ligi dhidi ya wapinzani wao, Real Madrid.
Akizungumzia umuhimu wa Raphinha katika kikosi, Flick alisisitiza kujituma na uongozi wa mchezaji huyo, huku pia akigusia upatikanaji wa wachezaji wengine, akiwemo Lamine Yamal ambaye ni majeruhi.
“Rapha daima anatoa asilimia 100,hiyo ndiyo fikra (mentality) yake, na mtazamo wake. Anatupa msaada mkubwa, lakini amepitia wakati mgumu msimu huu. Ni muhimu kuwa naye tena. Atasafiri na tutaona kitakachotokea. Yeye ni nahodha. Labda atatupa kile tunachohitaji.”Amesema kocha huyo wa Barcelona.





