Rarais wa Comoro ampa mwanae wa kiume ulaji serikalini
Eric Buyanza
July 3, 2024
Share :
Rais wa Comoro Azali Assoumani amemteua mwanae wa kiume Nour El Fath kuwa msimamizi wa kuratibu wa masuala ya serikali wakati alipolifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri siku ya Jumatatu kufuatia uchaguzi wa Januari ambao wapinzani wake walidai uligubikwa na udanganyifu.
Wachambuzi wa kisiasa, viongozi wa upinzani na vyombo vya habari nchini humo wanasema Rais Assoumani anaonekana dhahiri kumuandaa mwanae El Fath mwenye umri wa miaka 40 kuchukua nafasi yake.
El Fath ni msomi aliyebobea kwenye masuala ya fedha na aliyefanya kazi kama mshauri mwandamizi wa kiuchumi wa rais huyo tangu mwaka 2019.