pmbet

Rashford alimwa faini Bilioni 2 kisa kwenda klabu usiku

Sisti Herman

January 29, 2024
Share :

Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford anakabiliwa na adhabu ya faini ya pauni laki sita na nusu (£650,000) baada ya kunaswa akijirusha katika klabu ya usiku siku ya Alhamisi kabla ya kuripoti akiwa anaumwa siku inayofuata hali iliyopelekea kukosa mchezo wa kombe la FA  dhidi ya Newport County.

Akizungumzia kutokwepo kwa nyota huyo raia wa England baada ya ushindi wa 4-2 dhidi ya Newport, meneja Eric Ten Hag amesema hili ni suala la ndani na kwamba atalishughulikia binafsi.

Jarida la The Sun linaripoti Man United sasa wameamua kumtoza Rashford faini hiyo ya zaidi ya Tsh bilioni 2 ambayo ni sawa na mshahara wake wa wiki mbili kutokana na kujirusha katika usiku ya Belfast huko Ireland Kaskazini.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet