Rashford ana Tatoo ya namba za jezi alizovaa akiwa Man United
Eric Buyanza
June 3, 2026
Share :
Tambua tu kwamba Marcus Rashford amechora Tatoo ya nambari tofauti za jezi alizovaa akiwa Manchester United.
Marcus Rashford amewahi kuvaa rasmi jezi za namba tatu tofauti:
Namba 39: Hii ndiyo namba aliyoanza nayo wakati anapandishwa rasmi kwenye kikosi cha kwanza msimu wa 2015/16 chini ya kocha Louis van Gaal, na aliitumia kufunga magoli yake ya kwanza ya mapema.
Namba 19: Alikabidhiwa namba hii kuanzia msimu wa 2016/17 hadi 2017/18 baada ya kuanza kuwa mchezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza.
Namba 10: Alipewa jezi hii ya heshima msimu wa 2018/19 chini ya kocha Jose Mourinho (baada ya kuondoka kwa Zlatan Ibrahimović) na alidumu nayo kwa misimu mingi.





