Rashford kurejea Man U Barcelona yakwama kumnunua.
Joyce Shedrack
June 10, 2026
Share :
Klabu ya FC Barcelona inaripotiwa kukataa kutumia kipengele chake cha kulipa pauni milioni 30 sawa na Bilioni 104 za Kitazania ili kumsajili moja kwa moja mshambuliaji Marcus Rashford kutoka Manchester United msimu huu wa joto.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England tayari ameondoa kumbukumbu yoyote ya klabu hiyo ya Catalonia kwenye wasifu wake wa Instagram.
Rashford, mwenye umri wa miaka 28, sasa anatarajiwa kurejea Manchester United baada ya Kombe la Dunia la majira haya ya joto, isipokuwa klabu hiyo ifanikiwe kupanga uhamisho wake kwenda timu nyingine yoyote inayomhitaji kabla ya hapo huku kipengele cha Barcelona kumsajili moja kwa moja kinadaiwa kuisha siku ya Jumatatu.
Mabingwa wa Hispania wameonekana kumchagua Anthony Gordon badala ya Rashford wakikamilisha usajili huo kwa pauni milioni 60 sawa na Bilioni 210 za Tanzania kwa Gordon kutoka Newcastle United mwishoni mwa mwezi uliopita.





