pmbet

Rashford kwenye Penzi jipya na mwanamitindo

Sisti Herman

May 1, 2024
Share :

Gazeti la The Sun la nchini Uingereza limeibua tetesi za mchezaji wa klabu ya Manchester United, Marcus Rashford kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamitindo kutoka nchini Colombia, Erica Correa baada ya hivi karibuni kuonekana wakiwa pamoja katika kumbi za starehe.

Wawili hao wamekuwa gumzo mitandaoni ambapo baadhi ya watu wana hisi huwenda wakawa katika mahusiano ya kimapenzi.

Rashford mwenye umri wa miaka 26 alionekana akiwa na mwanamitindo huyo mzaliwa wa Colombia kwenye ukumbu wa starehe katika jiji la Manchester nchini Ungereza siku ya Jumapili jioni.

Inadaiwa kuwa nyota huyo wa Man United tangu alipoachana na mpenzi wake Lucia Loi mwaka 2023 hakuwahi kuonekana na mwanamke kwa ukaribu hivyo kama alivyo kuwa na mwanamitindo huyo.

Rashford na Lucia Loi walianza kuwa katika mahusiano miaka nane iliyopita wakiwa na umri wa miaka 15 wakiti wapo shule ya Aston iliyopo Manchester na kuachana mwaka 2023.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet