pmbet

Rashidi aua mkewe kwa kumyonga na mikono, kisha na yeye kujiua

Eric Buyanza

February 22, 2024
Share :

Rashidi Mkayala mkazi wa Mtaa Gemu Kata ya Mwanga Kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji amemuua mke wake Bernadeta Cosmas kwa kumnyonga shingo hadi kufa chanzo kikielezwa kuwa ni mgogoro wa vitu vya ndani alivyouza bwana Rashidi.
 

Muda mfupi baada ya Mkayala kutekeleza tukio la kumnyonga mkewe, naye alijinyonga kwa kutumia kilemba cha kuvaa kichwani.

Akielezea chanzo cha tukio hilo lililotokea usiku wa kuamakia jana Februari 21, 2024, Mwenyekiti wa mtaa huo, Buswalu Mkama amesema chanzo ni mgogoro uliotokea siku za nyuma ambapo mke wa marehemu alifika kwa mwenyekiti huyo na kutoa taarifa ya vitendo vya mume wake kuuza vitu vya ndani bila makubaliano baina yao.
 

Amesema amekuwa akisuluhisha kesi za wanandoa hao ambazo zimekuwa zikiripotiwa katika ofisi yake mara kadhaa kwaajili ya kutafutiwa ufumbuzi na kuondoa changamoto.
 

“Siku moja kabla ya tukio Bernadetha alilala nyumbani kwangu baada ya kumkimbia mumewe kutokana na kipigo alichokipata, alinusurika kuuawa kwa kunyongwa na waya wa umeme, alipopata nafasi ya kuchomoka alikimbilia kwangu ambapo alilala na kuondoka kesho yake (siku ya tukio)” ameeleza mwenyekiti huyo.
 

Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa marehemu Rashid alimnyonga mkewe kwa mikono hadi kumuua na baadaye kutoka nje ambapo alifunga mlango kwa nje na kurudi ndani kwa kupitia dirishani ambapo alifunga milango yote na madirisha na yeye kujinyonga kwa kitambaa cha kichwani.
 

Hadi sasa miili ya wanandoa hao imehifadhiwa kwenye hospitali ya mkoa ya rufaa ya Maweni wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelezwa na jeshi la polisi.
Nipashe

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet