Rasmi Cristiano Ronaldo kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya 6.
Joyce Shedrack
May 19, 2026
Share :
Nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo amejumuishwa kwenye kikosi cha Taifa lake kitakachoshiriki Kombe la Dunia 2026.
.jpg?auto=webp&format=pjpg&width=3840&quality=60)
Ronaldo ameitwa kwenye kikosi hicho huku ikiwa ni mara ya 6 kuipeperusha bendera ya Taifa lake kwenye michuano hiyo.
Nyota huyo alianza kuitwa kwenye kikosi cha Kombe la Dunia mara ya kwanza kwenye michuano ya mwaka 2006 yaliyofanyika Ujerumani mara ya pili 2010,2014, 2018,2022 na mwaka huu 2026.





