pmbet

Rasmi: John Stones atua Inter Milan

Eric Buyanza

July 31, 2026
Share :

Beki wa kimataifa wa England, John Stones, amejiunga na mabingwa wa Italia Inter Milan kwa uhamisho wa bure na kusaini mkataba wa miaka miwili.

 

Stones mwenye umri wa miaka 32 ameondoka Manchester City baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa mwezi Juni, akihitimisha safari ya mafanikio ya miaka 10 ndani ya klabu hiyo.

 

🗣️ "Nimeishi ndoto zangu zote," amesema Stones, baada ya kutwaa mataji mengi akiwa City, yakiwemo:

🏆 Ligi Kuu England mara 6
🏆 Ligi ya Mabingwa Ulaya mara 1
🏆 FA Cup mara 2
🏆 Carabao Cup mara 5
🏆 Community Shield mara 3
🏆 Kombe la Dunia la Klabu
🏆 UEFA Super Cup

 

Baada ya kuwa mchezaji huru, Stones alivutia vilabu kadhaa vikubwa barani Ulaya, ikiwemo Chelsea na Juventus, kabla ya kuamua kujiunga na Inter Milan.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet