pmbet

Rayvanny alamba dili nono U.S.A

Sisti Herman

February 25, 2024
Share :

Msanii maarufu wa muziki nchini Rayvanny, amesaini mkataba wa mamilioni ya fedha nchini Marekani, kuzindua aina mbalimbali za manukato yake ya wanaume na wanawake mwaka huu, ambapo ataungwa mkono na kampeni kubwa ya matangazo ya Kimataifa.

Rayvanny maarufu kama Chui anaingiza sokoni bidhaa yake ya manukato iitwayo "Fleur By Rayvanny" ambapo inakuja kutokana na msukumo mkubwa wa jina la EP yake ya 2020, "Flowers".

Fleur By Rayvanny itakuwa bidhaa ya kwanza katika mkataba huo na manukato hayo ambayo ni kwaajili ya jinsia zote yatauzwa mtandaoni na madukani ulimwenguni kote.

Rayvanny ameingia Mkataba na Nankoung Inc kwa kushirikiana na kampuni ya Kempt man, ambayo huzalisha Pafyumu na bidhaa za urembo kwa watu wengine maarufu duniani kuleta "Fleur By Rayvanny" mwaka huu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet