Rayvanny ndo msanii hatari kwenye "Remix" - Chino
Sisti Herman
January 19, 2024
Share :
Msanii wa muziki wa bongo fleva hapa nyumbani Tanzania Chino Kidd amesema hakuna anayepaswa kumdharau msanii Rayvany kwa sababu ni msanii mwenye moyo wa upendo na anapenda kusaidia watu hadi kujitolea kufanya “Remix” .
Chino amezungumza hayo jana usiku kwenye shughuli ya Royal birthday na Engagement ya Haji Manara na mpenzi wake Zaylissa, Chino ameweka wazi kuwa Rayvan ni msanii wa tofauti na yeye ni mmoja wa shabiki yake.
Kuhusiana na ngoma yake ya Gibela Chino amesema yeye ndiye aliyemfata Rayvany na alitamani awepo kwenye huo wimbo haya hapa maneno ya Chino.
"Niliamini kwenye Gibela yeye ndiye anayeweza kufanya remix kuwa bora na mmeona imefanya vizuri na inaendelea kufanya vizuri" amesema Chino,
Hata hivyo, Msanii Chino amemaliza kwa kusema ana mheshimu sana Rayvany na amemtaka kutokukata tamaa na asiache kusaidia watu kwani yeye pia kuna watu amewasaidia lakini wanamsema vibaya.