RC mpya wa Arusha asisitiza upendo,Amani na Mshikamano.
Joyce Shedrack
July 1, 2025
Share :
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Kenan Laban Kihongosi @kenanikihongosi amewataka watumishi wa Umma kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano na sio kufanya kazi kwa mashindano, kwa kutambua wote wanajenga nyumba moja, ili mmoja akiwa bora wote wawe bora na Arusha iwe salama ya upendo amani na mshikamano na kubainisha kuwa, hapendezwi kuona watu wakiharibikiwa kwenye maisha yao ya kazi.
Mhe. KIihongosi ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuwaapisha wakuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Gloriana Julius Kimath na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Mwinyi Ahmed Mwinyi, ikiwa ni jukumu lake la kwanza mara baada ya kukabidhiwa Ofisi, Juni 30,2025.
Amesema kuwa, kila mtumishi anawajibu wa kuwatumikia wananchi kwa kufanya kazi kwa weledi mkubwa kwa kushirikiana na kusaidiana na wengine ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kuwaletea wananchi maendeleo na kuacha na tabia ya mashindano kwa wote wanatekeleza dhamana waliyopewa na kuaminia na Serikali.
"Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kuthaminiwa bila kujali hali yake, kama viongozi tunao wajibu wa kuwahudumia watu kwa heshima kwa kuzingatia Kanuni, heria na taratibu za Utumishi wa Umma, tusipende kuonea watu, kwa kuwa kila mtu ana nafasi yake, tutambue kuwa tumekutanishwa kwenye kazi kwa kusudi ya Mungu, hivyo majungu na fitina hazina nafasi baina yetu".Amebainisha Mhe.Kihongosi.
Amesisitiza kuwa, katika kufanya kazi kwake, majungu na fitina viwe mwiko, kuwa hataweza kumhukumu mtu bila kufanya nae kazi, na kuongeza kuwa anatamani kuwafahamu watu kwa uwajibikaji wao anapofanya nao kazi na sio kuambiwa maneno na mtu na mtu mwingine.
"Tusaidiane, tuhurumiane, tuheshimiane, tuambiane ukweli kwa nidhamu, kila mtu awe baraka kwa mwingine, tusifurahie wengine wakiharibikiwa, tuwe baraka kwa watu wote, kila mtu afanye kazi kwa kutambua thamani ya mwingine kwa kuwa tunajenga nyumba moja, tuweke mbali chukii huku kipaumbele chetu kikiwa ni kutatua migogoro na changamoto za wananchi wetu ili kazi iendelee.