RC Mtanda awa mbogo atoa siku 7 Milioni 15 ziwasilishwe benki.
Joyce Shedrack
June 13, 2024
Share :
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ametoa muda wa Siku 7 kwa watumishi wanaokusanya mapato wa halmashauri ya Wilaya ya Magu kuhakikisha wanawasilisha fedha zaidi ya Tshs. Milioni 15 benki na wasipotekeleza hayo watawachukulia hatua za sheria.
Mhe. Mtanda ametoa agizo hilo leo tarehe 13 juni, 2024 wakati akizungumza na baadhi ya wazee, wadau wa maendeleo pamoja na watumishi wa Halmashauri na kubaini kuwa Halmashauri hiyo imekusanya mapato ya ndani kwa 87% tu kwa mwaka unaoishia juni 30, 2024.
"Halmashauri yenu haifanyi vibaya lakini haijafikia malengo ya ukusanyaji wa wapato ya ndani, naelekeza siku chache zilizobakia halmashauri ifikishe asilimia mia na kwa wanaodaiwa zaidi ya milioni 15 ndani ya siku 7 wawasilishe benki fedha hizo." Mkuu wa Mkoa.
Mtanda ameeleza kuwa ni lazima kuwe na uzingatiaji wa sheria kwenye ukusanyaji pamoja na matumizi ikiwemo upelekaji wa fedha za mapato ya ndani kwenye miradi ya maendeleo ili wananchi wapate huduma za kijamii zilizoboreshwa.