pmbet

Real Madrid kumchomoa Diogo Dalot Manchester United.

Joyce Shedrack

December 3, 2024
Share :

Klabu ya Real Madrid imewasiliana na wawakilishi wa beki wa kulia wa Timu ya Taifa ya Ureno na klabu ya Manchester United Diogo Dalot mwenye umri wa miaka 25 ili kuipata huduma ya nyota huyo wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi januari.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinaeleza kuwa Madrid wamejibiwa kuwa Manchester United itahitaji zaidi ya Bilioni 166 ili kumuachilia Dalot ambaye amekuwa msaada mkubwa kwenye kikosi cha United na mkataba wake utatamatika june 2028.

 

Real Madrid wamefikiria kumsajili Dalot badala ya beki wa Liverpool na Uingereza Trent Alexander-Arnold 26 ambaye alikuwa chaguo lao la kwanza ila wanaona hawataweza kusubiri mpaka atakapomaliza mkataba wake wa mwaka mmoja uliosalia ndani ya Liverpool.

 

Ikumbukwe, kuwa Real Madrid wanatafuta mbadala wa beki wao wa kulia Dani Carvajal atakayekosekana msimu mzima baada ya kupata jeraha baya la goti mwanzoni mwa msimu huu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet