Real Madrid kuumuza Carreras kwa Arsenal
Eric Buyanza
May 6, 2026
Share :

Real Madrid wako tayari kumuuza Alvaro Carreras kwa klabu ya Arsenal katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, hii ni kulingana na ripoti za nchini Hispania.
Mnamo Aprili 29, tovuti ya CaughtOffside iliripoti kuwa kocha wa Arsenal Mikel Arteta 'anataka' kumsajili Carreraso.
Ripoti ilidai kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United mwenyewe yuko tayari kuhamia Arsenal, ambao wamefika fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu na pia wako kileleni mwa jedwali la Ligi kuu nchini Uingereza.
Alvaro Carreras beki wa kushoto mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na Madrid akitokea Benfica mwaka 2025 kwa paundi milioni 43.1.





