Real Madrid Wagomea Bilioni 56 za Kombe la Dunia 2025.
Sisti Herman
June 10, 2024
Share :
Klabu ya Real Madrid imepanga kugoma kushiriki Kombe la Dunia la Vilabu lililopangwa kufanyika kuanzia june 15 hadi julai 13,2025 Nchini Marekani wakidai kuwa mapato yatakuwa ni madogo kwa klabu kubwa kama hiyo.
Mapato ya mashindano hayo ni Euro 20m sawa na Bilioni 56 za kitanzania.
Kocha Mkuu wa Klabu hiyo Carlo Ancelotti amefunguka kupitia mahojiano yake na gazeti la Il Giornale:
"Real Madrid haitashiriki Kombe la Dunia la vilabu, tutakataa mwaliko wao".
"Mechi moja ya Real Madrid ina thamani ya €20m wao wanataka kutupa pesa hizo kwa shindano zima… hapana”, amesema Ancelotti .