Real Madrid watwaa Ubingwa wa Uefa kwa kuwachapa Dortmund
Sisti Herman
June 2, 2024
Share :
Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania jana usiku imetwaa taji la ligi ya Mabingwa baada ya kuwafunga 2-0 Borussia Dortmund ya Ujerumani kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye dimba la Wembley jijini London Uingereza.
Kwenye mchezo huo, magoli ya Madrid yalifungwa na Dani Carvajal aliyemalizia kona iliyopigwa na kiungo mjerumani Toni Kroos huku lingine likifungwa na mshambuliaji hatari wa Brazil Vinicius Junior aliyepikiwa na kiungo wa Uingereza Jude Bellingham.
Huo unakuwa Ubingwa wa 15 kwa Real Madrid, ikiendelea kushikilia usukani wa kuwa na mataji mengi a Uefa.