pmbet

Real Madrid yatupa karata ya mwisho kumnyakua Mbappe

Eric Buyanza

December 30, 2023
Share :

Real Madrid wamefanya jaribio jingine la kumsajili Kylian Mbappe kutoka Paris Saint-Germain na wamempa mchezaji huyo muda wa kuamua kama anataka kujiunga na klabu hiyo.

Kuanzia Januari 1, Mbappe atakuwa katika miezi sita ya mwisho ya mkataba wake na PSG, hivyo atakuwa huru kufanya mazungumzo na vilabu vingine kabla ya uhamisho wa bure.

Real Madrid wameweka wazi kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kwamba, ikiwa anataka kujiunga nao lazima afanye maamuzi kabla ya katikati ya Januari.

Kila mtu Valdebebas anataka Mbappe aende kuimarisha timu, kuanzia kocha mkuu Carlo Ancelotti hadi kwa wachezaji akiwemo Vinicius Junior, ambaye anawasiliana sana na Mbappe.

Mbappe ana mawasiliano ya moja kwa moja na rais wa Real Madrid Florentino Perez, ambaye ni mfuasi mkubwa wa Mbappe.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet