Red Arrows mabingwa wapya wa Kagame Cup 2024.
Joyce Shedrack
July 21, 2024
Share :
Klabu ya Red Arrows ya Zambia imeibuka mabingwa wa CECAFA Kagame Cup baada ya kuitandika APR ya Rwanda kwa mikwaju ya penalti 10-9.
Kwenye mchezo huo wa Fainali Red Arrows walipata bao la kuongoza kipindi cha pili kabla ya APR kusawazisha bao hilo katika dakika 5 za nyongeza na kusababisha mchezo kufikia hatua za kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti na hii ni baada ya dakika 30 za nyongeza kushindwa kupatikana goli kwa timu zote .
Hii inakuwa mara ya kwanza kwa klabu hiyo kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.