"Reece James ni beki bora zaidi wa kulia Duniani"-Rosenior.
Joyce Shedrack
March 14, 2026
Share :
Kocha mkuu wa Chelsea FC, Liam Rosenior, amesema klabu hiyo “imepata mchezaji bora zaidi duniani katika nafasi yake” baada ya beki wa kulia Reece James kusaini mkataba mpya wa miaka sita.

James, mwenye miaka 26, alijiunga na timu kubwa ya Chelsea na kucheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha wakubwa mwezi Septemba 2019 akitokea timu ya vijana ya ‘the blues’.
Rosenior alisema hawezi kuacha kutabasamu kutokana na habari kwamba James ataendelea kubaki klabuni kwa muda mrefu, “Siwezi kuacha kutabasam Reece James amesaini mkataba mpya na tumehakikisha mchezaji bora zaidi duniani katika nafasi yake anaendelea kubaki hapa!”
“Alikuwa na fursa nyingi za kuondoka katika klabu hii,” alisema Rosenior, ambaye alimrithi Enzo Maresca katika uwanja wa Stamford Bridge mwezi Januari".
“Sio tu kuhusu ukubwa na hadhi ya klabu aliyokulia, bali pia ni kuhusu imani na kujiamini kwake katika kile tunachokifanya na tunakotaka kufika. Tumekuwa na mazungumzo mengi kuhusu hilo ,Kwa yeye kusaini mkataba na kuweka imani yake kwetu ni hatua kubwa sana.”Amesema Rosenior.





