Refa alivyowaua Madrid na kumlima Bellingham Nyekundu
Sisti Herman
March 3, 2024
Share :
Maamuzi ya marefarii yameendelea kuwa doa kwenye ligi mbalimbali barani Ulaya baada ya jana mwamuzi Jesus Gil Manzano kupuliza kipenga cha kumaliza mchezo wakati kiungo mshambuliaji wa Real Madrid akimalizia kwa kichwa na kuweka mpira nyavuni mpira wa krosi iliyopigwa na Brahimi na ambao ulikuwa kwenye na mwendo kuandika bao la kuongoza kwa Real Madrid dhidi ya Valencia kwenye mchezo wa La Liga uliotamatika kwa sare ya 2-2.
Baada ya tukio hilo ambalo kila mdau wasoka alilitafsiri kuwa la hovyo kuwahi kutokea, wacjezaji wa madrid walimzonga mwamuzi huyo hadi ikapelekea Bellingham kupata kadi nyekundu baada ya mchezo.
Mabao ya Madrid kwenye mchezo huo yalifungwa na winga hatari zaidi kwasasa duniani Vinicius Jr kabla ya hilo la Bellingham lililokataliwa a mwamuzi.